
Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC na Baraza la Habari Tanzania MCT wameweka bayana malalamiko yao kuwa Tanzania imeendeleza ukandamizaji dhidi ya vyombo vya habari na waandishi wa habari.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Dr. Anna Henga wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kimaraifa ya uhuru wa vyombo vya habari yanayofanyika mjini Arusha

Dr. Henga ameweka bayana kuwa kuwekuwepo na matumizi mabaya ya mamalaka za serikali kuzuia waandishi wa habari kufanya kazi zao pamoja na kufungia vyombo vya Habari akibainisha kuwa katika kipindi cha January hadi April mwaka huu takribani matukio manane ya ukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya Habari yameripotiwa
Anasisitiza kuwa uhuru wa kujieleza, haki ya kupata, kuchakata na kuwasilisha habari inayotambuliwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18 imekiukwa na utamaduni wa kuvumiliana kati ya vyombo vya Habari na serikali unatoweka kutokana na sheria zinazotungwa kwenda kinyume na ibara hiyo ya Katiba.
Awali Katibu wa Baraza la Habari Tanzania Ernest Sungura akitoa taarifa ya pamoja ya taasisi na mtandao wa kutetea haki ya kupata habari nchini Tanzania CoRi ametaja kuwa tayari taifa kimerekodi matukio mengi ya kukamatwa kwa waandishi wa Habari, kunyanganywa vitendea kazi na kufungia vituo vya Habari akitaja tukio la hivi karibuni la kufungiwa kwa siku 90 kituo cha runinga mtandaoni cha Jambo TV.
Hata Hivyo Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maudhui ya mamalaka ya mawasiliano Tanzania Bw, Issac mruma amekanusha madai ya ukandamizaji akieleza kuwa wanaofungiwa vyombo vyao ni baada ya kubainika kuwa na makosa yanayojirudia na hupewa nafasi ya kujieleza, kujitetea na wakati mwingine wanaonywa kabla ya uamuzi wa kufungia vyombo vyao
Mruma amebainisha kuwa, serikali ya tanzania inazingatia misingi ya uandishi wa Habari na utangazaji na inathamini mchango wa vyombo vya Habari nchini humo na kwamba ni wajibu wa waandishi wa Habari na vyombo husika kuzingatia maadili na sheria zilizoainishwa kusimamia tansnia hiyo mhimu.

Tanzania leo imezindua wiki ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari ambayo kitaifa yanafanyika mjini Arusha na katika ngazi ya Afrika yatafanyika mjini Lusaka nchini Zambia May 03.

Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani afrika zinazosifika kwa kuwa na vyombo vingi vya Habari na utangazaji ikiwemo mitandao ya kijamii, radio na runinga mtandaoni, magazeti na vituo rasmi vya Runing ana Radio ambako kila mkoa unatajwa kuwa na kituo cha Radio kimoja au zaidi cha RADIO







